Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu inatarajiwa kuendelea kuunguruma leo huku mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi katika sehemu ya kwanza ya pingamizi la mshtakiwa mwenza na Mbowe.
Leo Jumanne Desemba 14, 2021 Jaji Joachim Tiganga wa Mahakama ya Kuu, Divisheni ya Makosa ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, anatarajia kutoa uamuzi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi kutokana na upande wa utetezi kuweka pingamizi kuhusiana na malezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Mohamed Ling'wenya.
Mawakili hao wa upande wa utetezi walipinga maelezo hayo yaliyotolewa na SP Jumanne yasipokelewe na mahakama kwa sababu mshtakiwa huyo alilazimishwa kusaini na wala hajawahi kufikishwa kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
Tayari washtakiwa tayari wameshafikishwa mahakamani kwa ajili ya kuendelea na kesi hiyo.
Pia, awakili wa pande zote mbili nao wameshafika katika Mahakama kwa ajili ya kusikiliza uamuzi katika kesi ndiogo ndani ya kesi ya msingi.
Kwa sasa anayesubiriwa ni Jaji Tiganga kuingia mahakama
Advertisement Mbowe na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi.
SOMA: Mwelekeo wa uamuzi kesi ya kina Mbowe
Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo katika maeneo Moshi, Arusha na Dar es Salaam.
Kama kawaida Mwananchi itaendelea kukuletea mwenendo wa kesi hii moja kwa moja “Live Updates” kutoka mahakamani hapo kadri kesi itakavyokuwa inaendelea.