Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu kesho inatarajiwa kuendelea kuunguruma huku mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi katika sehemu ya kwanza ya pingamizi la mshtakiwa mwenza na Mbowe.
Hizi ndizo hoja za sehemu ya pili ya pingamizi hilo ambazo zinasubiri kusikilizwa leo iwapo mahakama itatupilia mbali hoja zitakazoamuriwa leo
1: Maelezo hayo yamerekodiwa chini ya sheria isiyokuwepo yaani marekebisho ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), ya mwaka 2018.
2: Mshtakiwa alionywa chini ya sheria isiyo sahihi yaani Sheria hiyo ya mwenendo wa Jinai, Marejeo ya mwaka 2018 na pia Sheria ya Kupambana na Ugaidi (combating terrorism) badala ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi (Prevetion of terrorism).
3: Hakuna onyo kwa kuwa kifungu cha 24 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi kilichotumika kumuonya, kutokana na kutokuwepo kwa kifungu kidogo cha (2), kunamanya mshtakiwa asijue kuwa anaonywa kwa kosa la kutenda vitendo vya kigaidi wapi (Nje au ndani ya nchi)
4: Nyaraka hiyo (inayodaiwa kuwa maelezo ya mshtakiwa) haijakidhi vigezo vya kuwa maelezo ya onyo, kwa kuwa anayeonywa anapoanza kukiri anatakiwa apewe onyo la pekee kwa kumpeleka mbele ya Mlinzi wa Amani (hakimu yeyote wa Mahakama ya Mwanzo)