Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KESI YA KINA KITILYA:Mchumi aeleza jinsi mkopo wa dola 550 milioni ulivyopitishwa na Waziri wa Fedha

77347 Mchumipic

Thu, 26 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mchumi mwandamizi katika Idara ya Sera Kitengo cha Sera na Madini, Moris Linuma ameieleza Mahakama Kuu kuwa pendekezo la mkopo wa dola 550 milioni za Kimarekani lilipitishwa na Waziri wa Fedha Septemba 25, mwaka 2012.

Mkopo huo ni ule wenye ada ya asilimia 2.4 ulioshughulikiwa na benki ya Stanbic Tanzania na Standard ya Afrika Kusini kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ya mwaka 2012/2013.

Linuma, ambaye ni shahidi wa nane wa upande wa mashtaka, alieleza hilo jana wakati akihojiwa na wakili wa utetezi, Zaharani Sinare kuwa atakuwa sahihi akisema pendekezo la mkopo huo lilipitishwa na Waziri wa Fedha Septemba 25, 2012.

Alikuwa akijieleza mbele ya Jaji Emmaculata Banzi wakati wa usikilizwaji wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwenyekiti wa kampuni inayoshughulikia uwekezaji wa mitaji na dhamana ya Egma, Harry Kitilya na wenzake wanne.

Mbali na Kitilya, washtakiwa wengine ni Shose Sinare, Sioi Solomon, Bedason Shallanda na Alfred Misana.

Wakili Sinare alimuhoji shahidi huyo kama anakumbuka kikao cha 62 cha kamati ya kiufundi inayoshughulikia madeni ya serikali (TDMC ) kilichofanyika Septemba 25, 2012.

Pia Soma

Advertisement
Akijibu hoja hiyo, Linuma alikubali kuwa kilifanyika.

Sinare: Utakubaliana na mimi kuwa kikao cha TDMC kilikaa siku hiyo hiyo ya Septemba 25, 2012, siku ambayo Waziri alipitisha mkopo wa dola 550 milioni.

Linuma: Ni kweli.

Sinare: Utakubaliana na mimi kwa kuwa mkopo huo wa dola 550 milioni ulishapitishwa na Waziri Septemba 25,2012 na haukupaswa kujadiliwa tena kwenye kikao cha 62 cha TDMC.

Linuma: Sidhani kama itakuwa sahihi kwa sababu iliishaamuliwa ujadiliwe katika kikao kinachofuata.

Sinare: Inawezekana pendekezo lililokwishakubaliwa na waziri likajadiliwa tena na kikao cha TDMC.

Linuma: Haiwezekani.

Sinare: Shahidi unakumbuka ulisema hujui sababu ya pendekezo la mkopo wa dola 550 milioni la Agosti 2,2012 halikujadiliwa kwenye kikao cha 62 cha TDMC.

Linuma: Kimya

Sinare: Sasa unijibu umeishasema pendekezo la mkopo la Agosti 2,2012 lilipitishwa na waziri Septemba 25,2012 na kikao cha TDMC kilikaa siku hiyo hiyo, hivyo isingewezekana kikao hicho cha 62 kulijadili kwa sababu lilikwishapitishwa na waziri?

Linuma: Ni kweli isingewezekana kujadili kwa sababu lilikwishapitishwa na waziri.

Sinare: Unakumbuka kikao cha 46 cha kamati ya taifa inayoshughulikia madeni ya serikali (NDMC) kilikaa siku gani.

Linuma: Kilikaa Septemba 19,2012.

Sinare: Utakumbuka mojawapo ya mapendekezo ya kikao hicho benki ya Stanbic ya Tanzania na Standard walishauriwa wapeleke barua ya ridhaa (mandate letter) ili Serikali ipitie.

Linuma: Ni moja ya mapendekezo.

Barua ya ridhaa ni ile ambayo anapewa mkopeshaji na mkopaji ili aweze kwenda kutafuta fedha kwa muda maalum na kwa masharti watakayokubaliana na ni lazima yasainiwe na pande zote mbili.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 58, yakiwemo ya kuisababishia Serikali hasara ya dola 6 milioni, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na utakatishaji.

Chanzo: mwananchi.co.tz