Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KENYA: Mamia ya wanafunzi wachomana visu katika vurugu za kidini Kenya

1841 DUSZvFHWsAIfbdK TZW

Thu, 25 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Mamia ya wanafunzi nchini Kenya katika shule ya Sekondari ya Jamhuri jijini Nairobi wapo katika hali mbaya ya kiafya baada ya usiku wa jana kutokea vurugu ya kidini kwenye shule hiyo.



Taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini Kenya zinaeleza kuwa wanafunzi hao walikuwa wakizozana kati ya Waislamu na Wakristo.

Kwenye mzozo huo Wanafunzi wa dini ya Kiislamu walikuwa wanawalazimisha wenzao wakristo kubadilisha dini (Kuslimu) na ndipo vurugu zilipoanzia.

Taarifa za awali zinaelezankuwa vurugu hizo zimetoa usiku wa kuamkia leo na mamia ya Wanafunzi wamejeruhiwa kwa kuchomwa visu huku vitanda na madawati yakivunjwa kwenye vurugu hizo.



Hata hivyo tayari Jeshi la Polisi jijini Nairobi limefika shuleni hapo asubuhi hii kufuatilia tukio hilo ili kutoa taarifa rasmi idadi ya wanafunzi waliojeruhiwa.

Chanzo: bongo5.com