Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

John atupwa jela miaka 15 kwa kutaka kumbaka bibi yake

Jela Miaka 60 Kwa Kumpa Mimba Mwanafunzi John atupwa jela miaka 15 kwa kutaka kumbaka bibi yake

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Lindi, imemuhukumu kwenda jela miaka 15 John Swaki Fokasi, kwa kosa la kujaribu kumbaka bibi kizee wa miaka 80.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Aprili 03, 2024 huko Tulieni mashambani majira ya saa sita usiku alipomvamia bibi kizee huyo kwenye nyumba aliyokuwa amejihifadhi na kuanza purukushani za kutaka kumuingilia kinguvu bila ridhaa yake, mpaka bibi kuzee huyo alipojiokoa kwa kumkata panga sehemu ya kichwani na mkoni ndipo mtuhumiwa huyo akakimbia kusiko julikana mpaka alipokamatwa siku iliyofuta na kufikishwa Mahakamani.

Hukumu hiyo ya kesi namba 10546/2024 imetolewa na Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Mhe.Deliphina Kimati ili iwe fundisho na kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live