Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joachim Tiganga jaji mpya kesi ya kina Mbowe

Jaji Tnganapic Joachim Tiganga jaji mpya kesi ya kina Mbowe

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, imepata Jaji mpya Joachim Tiganga

Jaji Tiganga amejitambulisha katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi mbele ya washtakiwa na upande wa mashtaka

Kesi hiyo imepangwa kuendelea tena leo Jumanne Oktoba 26, 2021 baada ya kusimama kwa siku saba, tangu Oktoba 20, huku Jaji Kiongozi Mustapha Siyani aliyekuwa akiisikiliza alipojitoa kutokana na kuongezewa majukumu.

Jana Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Ruswa na Uhujumu Uchumi inayosikiliza kesi hiyo ilitoa hati ya wito kwa pande zote katika kesi hiyo kufika mahakamani leo kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo.

Mbowe na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi

Chanzo: mwananchidigital