Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la zimamoto Arusha lilivyomuunga mkono Raisi JPM

2796 WhatsApp Image 2018 02 07 At 10.06.29 660x400.jpeg

Fri, 9 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo February 7, 2018 Jeshi la Zimamoto mkoani Arusha limekabidhi vifaa vya kuzimia moto, sita kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa niaba ya Rais John Magufuli kwaajili ya nyumba za polisi zilizojengwa Arusha.

Akikabidhi vifaa hivyo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamanda Kennedy Komba amesema Jeshi hilo lina wajibu wa kuhakikisha ujenzi wa nyumba za makazi unazingatia vigezo vyote vya usalama, wao kama Jeshi wanaunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuhakakikisha makazi ya askari polisi yanakua bora.

“Sisi kama Jeshi la Zimamoto na uokoaji tunaunga mkono jitihada za Amiri Jeshi Rais Magufuli sambamba na wadau wengine waliochangia ujenzi katika kuhakikisha nyumba hizi mpya za askari ambazo ziliungua moto miezi michache iliyopita zinakuwa salama kwa kuweka vizima moto katika kila nyumba kama matakwa ya usalama yanavyohitaji.” Kamanda Komba.

Naye RC Gambo amelipongeza sana jeshi hilo kwa kuonyesha moyo wa kujali jitihada za Rais na wao kufanya kitu ambacho kinatuma ujumbe kwa jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia usalama dhidi ya Majanga

Ujenzi wa nyumba hizo 31 kwaajili ya makazi ya askari polisi umetokana na janga la moto lililosababisha jumla ya kaya 13 za askari katika kituo kikuu cha Polisi mkoani Arusha kupoteza makazi na mali miezi michache iliyopita.

Mradi huu wa nyumba za polisi umegharimu zaidi ya shilingi milioni 540 ambapo shilijngi milioni 260 zimetolewa na Rais Magufuli.

“Tunawatia watu umasikini, hii sio haki” –Hussein Bashe



Ilivyokuwa kesi ya Mbunge Nasari Arusha



 
Chanzo: millardayo.com