Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la polisi linamsaka aliyekutwa na kichwa cha Pundamilia

Wanteddddddd Jeshi la polisi linamsaka aliyekutwa na kichwa cha Pundamilia

Sat, 13 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKAZI wa Kijiji cha Sarawe, Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Khamis Boman anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kukutwa na kichwa cha pundamilia nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Linginus Tibishubwamu akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake alisema kichwa hicho kilikutwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo Oktoba 21, mwaka huu.

Alisema askari wakiwa katika doria kama sehemu ya shughuli zao za kila siku, walipata taarifa kuhusu alipokuwa Boman anayetuhumiwa kwa wizi wa mifugo.

“Alipoona askari alitoroka na kutokomea kusikojulikana, askari waliingia ndani ya nyumba yake kwa ajili ya kufanya msako na katika hali isiyokuwa ya kawaida walikuta kichwa cha pundamilia kibichi,” alisema Tibishubwamu.

Tibishubwamu alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mara kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu badala yake watumie fursa zilizo kwenye mkoa huo ambao aliuelezea kuwa una utajiri wa kutosha.

Alisema Mara ni tajiri kutokana na kuwa na ardhi inayofaa kwa kilimo, uvuvi na madini na kwamba mtu anaweza kutajirika kwa haraka badala ya kuhatarisha usalama wake na familia kwa ujumla kwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live