Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Polisi limeripoti kuuwawa kwa Mwanamke Rombo

4545HBGG Jeshi la Polisi limeripoti kuuwawa kwa Mwanamke Rombo

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: millardayo.com

Polisi Mkoani Kilimanjaro wanamtafuta Mwanaume mmoja aliyesababisha mauaji ya Mke wake kutokana na ugomvi ambao ulitokea baada ya Mke huyo aitwae Fausta Silayo (22) kukataa kurudiana nae.

Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Simon Maigwa ameiambia Amplifaya ya Clouds FM kwamba “Majirani wamesema mgogoro ulitokea baina ya wawili hao na Mwanaume alikua akilazimisha warudiane, walikua wametengana kwa muda na Mwanamke akarudi kwa Wazazi wao, huyu Mwanaume alikwenda kwao kuona kama wanaweza kusuluhisha lakini ikaonekana kwa matendo ya yule Mwanaume isingewezekana hivyo kwa hasira Mwanaume ndio akaamua kumchoma visu Mke wake”- Jeshi la Polisi

“Baada ya Mwanamke kupiga kelele Mwanaume akatorokea migombani na unajua Rombo ni mpakani mwa Kenya na Tanzania, ametorokea Kenya lakini tunaendelea kumsaka na tutamkamata kwasababu anafahamika, tunashirikiana na Interpol, Mwanamke alijeruhiwa lakini baadae akafariki”- Jeshi la Polisi

SHAHIDI KESI YA SABAYA ASHANGAA ALIYEMPIGA KUTOKUWEPO MAHAKAMANI

Chanzo: millardayo.com