Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Polisi lathibitisha kupokea Bunduki 228 za uhalifu

Suimbapic 1 Jeshi la Polisi lathibitisha kupokea Bunduki 228

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: mtanzania.co.tz

Serikali imesema jumla ya silaha 228 zimesalimishwa kwa Jeshi la Polisi huku akiliagiza Jeshi hilo kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015.Hayo

Hayo yamebainishwa leo Desemba 6, 2021 jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene na kusema kuwa kufanya hivyo nikuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza na kuruhusu Magobole kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za ulinzi katika jamii.

Waziri Simbachawene amewaambiwa Waandishi wa Habari kuwa hatua hiyo ni katika utekelezaji wa tangazo la msamaha kwa usalimishaji wa silaha haramu kuanzia Novemba 1 hadi 30, 2021.

“Kwa mchanganuo wa PISTOL 5 sawa na 2.2% ya silaha zote zilizosamilishwa, magobore 174 sawa na 76.3% ya silaha zote zilizosalimishwa, S/gun 38 sawa na 16.7% ya silaha zote zilizosalimishwa, Rifle 10 sawa na 4.4% ya silaha zilizosalimishwa na SMG 01 sawa na 0.4% ya silaha zote zilizosalimishwa.

“Pia imesalimishwa jumla ya mitutu 12 ambapo mitutu 11 imesalimishwa Mkoa wa Tanga na Mtutu 1 umesalimishwa Mkoa wa Mbeya.

“Kati ya silaha zilizosalimishwa imeonekana kuwa magobore ni asilimia 76.3 jambo linaloonesha kuwa tatizo la utengenezaji wa silaha za kienyeji yakiwemo magobore ni kubwa hapa nchini,”amesema Sibachawene.

Amesema kufuatia matokeo haya ya usalimishaji wa silaha haramu,Waziri Simbachawene amelielekeza Jeshi la Polisi kuangalia upya uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015 ili kuweka utaratibu wa kisheria wa kutengeneza na kuruhusu Magobole kwa kuwa silaha hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za Ulinzi katika jamii.

Pia, kufanya misako kwa kutumia taarifa za kiintelelijensia ili kuwabaini na kuwakamata wale wote wanaomiliki silaha kinyume na Sheria na kisha kuwachukulia hatua za kisheria.

Chanzo: mtanzania.co.tz