Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Polisi lakamata silaha 199, risasi 360

6c1867b1af16264f738665b988a0f4e4 Jeshi la Polisi lakamata silaha 199, risasi 360

Sat, 13 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha zinazokadiriwa kufika 199 na risasi 360, shukrani kwa ushirikiano unaotolewa na wananchi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo, SACP David Msime leo, imechanganua kuwa, silaha hizo ambazo zilikamatwa mwaka jana ni pamoja na AK47 10, Pistol 16, Shortgun 39 na magobore 134.

Msime amesema silaha hizo zilitumika kutekeleza uhalifu mbalimbali ikiwemo unyang’anyi, mauaji na ujangili huku zingine zikikamatwa kutokana na kumilikiwa kinyume cha sheria.

Aidha, Msime ametoa wito kwa wananchi na wadau wa usalama kuondelea kutoa ushirikiano kama walioutoa mwaka jana ili kuimarisha usalama wa nchi.

Chanzo: habarileo.co.tz