Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Polisi kuwasaka watuhumiwa 67 wa mifugo

46cb4eebb91e9043517b9ea5a7f4e640 Jeshi la Polisi kuwasaka watuhumiwa 67 wa mifugo

Wed, 27 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka watumishi wa wizara hiyo waliopo kwenye minada ya upili na mipakani kuacha urasimu mara moja wa utoaji wa vibali mbali mbali vya mifugo na mazao yake.

Ndaki ameagiza kupatiwa orordha ya watumishi hao na viongozi wao na muda waliohudumu katika ofisi hizo na kuwachukulia hatua za kinidhamu watakaobainika kwenda kinyume na utaratibu wa kazi.

"Nataka nipatiwe taarifa za watu hao kuanzia vyeo vyao, umri wao na muda waliohudumu kwenye minada husika ili tuweze kuboresha kwenye eneo kwa sababu utaratibu wa kufanya kazi kwa mazoea umeshapitwa na wakati." amesema Ndaki

Amesema ili kuhakikisha mifugo na mazao ya mifugo haitoroshwi kuelekea nchi za jirani, waziri huyo amemuagiza Katibu wa wizara hiyo anayeshughulikia Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel kuchambua ripoti hiyo na kuainisha mapendekezo yaliyotolewa ili sekta ya mifugo iweze kuwa na mchango mkubwa zaidi katika pato la taifa.

Aidha Ndaki ametaka pia ushirikiano kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika kutatua changamoto zinazowakabili wafugaji ili mifugo isikae muda mrefu wakati wa kusafirishwa kwenda sokoni.

Chanzo: habarileo.co.tz