Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Polisi Shinyanga lakamata Dawa za Kulevya

Screenshot 2021 05 28 At 10.52.36 660x400.png Jeshi la Polisi Shinyanga lakamata Dawa za Kulevya

Fri, 28 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Masunga Nindwa (36) mkazi wa Lunzwe Mkoani Geita na Peter Matiko mkazi wa Nyakato Mkoani Mwanza wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kupatikana na Dawa za Kulevya aina ya bangi Kilogramu 20 na mirungi Kilogramu 25.

Akizungumza waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo (ACP) Debora Magiligimba amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika matukio mawili tofauti baada ya kufanyika kwa msako mkali wa jeshi hilo ambao umefanikisha kukamatwa kwa dawa hizo.

Katika tukio la kwanza Masunga Nindwa alikamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani Kahama Mei 21 mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni ya Kalunde iliyopo katika Mtaa wa Nyasubi akiwa na debe mbili za bangi zenye uzito wa Kilogramu 20 huku akijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kamanda Magiligimba amesema kuwa katika tukio la pili Mei 21 mwaka huu majira ya asubuhi katika Kata ya Ibinzamata Peter Matiko alikamatwa na Jeshi hilo akiwa na mirungi Kilogramu 25 iliyokuwa imewekwa kwenye mabegi aliyokuwa anaisafirisha kwenda mkoani Singida.

“Jeshi la Polisi lilipata taarifa za kiintelijensia kutoka kwa wasamaria wema na kuanza kuafuatilia na kisha kufanikiwa kuwakamata na dawa hizo za kulevya, mtuhumiwa wa mirugi alikiri kutumia na kuuza dawa hizo upelelezi ukikamilika tutawafiksha mahakamani,” Magiligimba.

Sambamba na hilo Magiligimba amesema kuwa Jeshi hilo pia linamshikilia Elida Zakaria (19) mkazi wa Kagongwa kwa tuhuma za kukutwa na kete 111 za Dawa za Kulevya aina ya bangi zilizokuwa zimefungwa kwenye magazeti kwenye nyumbani kwa Lucia Luhende ambaye ndiye mmiliki wa dawa hizo.

“Tunatarajia kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa wote upelelezi ukikamilika na tunatoa rai kwa wananchi kuwafichua watu wanaouza na kusafirisha dawa za kulevya ambazo zimekuwa zileta athari kwenye jamii”, Magiligimba.

TAZAMA MSAFARA WA MWANA WA KIFALME ULIVYOINGIA IKULU AKIKUTANA NA RAIS SAMIA

Chanzo: millardayo.com