Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka sita kwa kumbaka mlemavu matatizo ya akili

9476 PIC+JE%253BLA TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pemba. Mahakama ya Mkoa wa Chakechake kisiwani hapa amemhukumu Omar Hamad Khamis (19) kifungo cha miaka sita jela baada ya kumtia hatiani na kosa la kumbaka mtoto wa miaka 17 mwenye ulemavu wa akili.

Mahakama hiyo imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi saba mbele ya hakimu Hussein Makame Hussein.

Hakimu Hussein kabla ya kutoa hukumu mshtakiwa huyo alimpa nafasi ya kujitetea, ambaye aliiomba mahakama kumwachia kwa kuwa ni kosa lake la kwanza.

Hata hivyo, Hussein alitupilia mbali utetezi huo na kumhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo cha miaka sita jela na kumlipa binti huyo fidia ya Sh400,000.

Awali, ilidaiwa na mwendesha mashtaka Ali Haidari alidai mshtakiwa alimuingilia binti wa miaka 17 mlemavu wa akili na kwamba, ni kinyume na kifungu cha 133 cha sheria ya adhabu namba 6 ya mwaka 2004.

Haidari aliiomba mahakama kumpa adhabu kali mshtakiwa kutokana na makosa hayo kuongezeka. Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 14, akikabiliwa na shtaka hilo miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi ni binti mwenyewe, mama mzazi, dada yake, mpelelezi na daktari.

Chanzo: mwananchi.co.tz