Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka miwili kwa kumchoma kisu kaka yake

MIEZI 18 JELA Jela miaka miwili kwa kumchoma kisu kaka yake

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu Hassan Issa, kwenda jela miaka miwili, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu tumboni bila kukusudia.

Hassan anadaiwa kumchoma kisu kaka yake, Ismail Issa, baada ya kuzuiliwa asiangue madafu yaliyokuwepo nyumbani kwako na badala yake aliambiwa asubiri nasi zikomae, ndiyo aaungue.

Zuio hilo la kuangua madafu lilipelekea purukushani na kuanza kushambuliana na ndipo Hassan alipochukua kisu na kumchoma kaka yake tumboni.

Hukumu hiyo, ilitolewa jana Jumatatu, Novemba 7, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga, wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi upande wa mashitaka.

Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Neema Moshi, ulimkumbusha mshtakiwa shtaka lake la kuua bila kukusudia ambapo alikiri kosa hilo.

Katika maelezo ya mshtakiwa huyo, inadaiwa Hassan aligombana na kaka yake baada ya kuzuiliwa asiangue madafu badala yake asubili nasi zikomae, ndipo mshitakiwa walianza kushambuliana kisha akamchoma tumboni na kisu

Baada ya kukiri kosa hilo Hakimu Ruboroga, alimtia hatiani kama alivyoshitakiwa na hivyo kuandaa hukumu.

Mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani upande wa mashtaka uliomba mahakama impe mshtakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye tabia kama hizo.

Kwa upande wake, wakili wa utetezi Godfrey Ambet, aliomba Mahakama impunguzie adhabu mshitakiwa huyo kwani aliua bila kukusudia kutokana na kauli za Ismail, hivyo kusababisha ugomvi.

Hakimu Ruboroga baada ya kusikiliza hoja hizo amemhukumu Issa kwenda jela miaka miwili jela.

"Kwa kuwa umekiri shtaka lako mwenyewe la kuua bila kukusudia, Mahakama hii inakuhukumu kifungo cha miaka miwili jela na kama hujaridhika na hukumu hii, haki ya kukata rufaa ipo wazi" amesema Hakimu Ruboroga.

Chanzo: Mwananchi