Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka miwili kwa kukutwa na bangi

Jelakwawizi. Jela miaka miwili kwa kukutwa na bangi

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu watu wawili kifungo cha miaka miwili jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi, zenye uzito wa kilo 59.59. Mahakama hiyo, pia imetoa amri ya ya kuteketezwa kwa dawa hizo za kulevya.

Waliohukumiwa ni wakazi wa Kibamba CCM, Scola Kashinde na James Shija, wahukumiwa adhabu hiyo baada kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ya kukiri kosa, ambapo kwa mujibu wa sheria mtu akipatikana hatia adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 gerezani.

Akitoka hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio; amesema mahakama hiyo imezingatia makubaliano yaliyoingiwa kati ya DPP na washitakiwa hao, na hivyo inawahukuku kifungo cha miaka miwili jela.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Machi 27, 2023 katika eneo la Kibamba CCM, Wilaya ya Ubungo, mkoani Dar es Salaam.

Inadaiwa kwamba, washitakiwa hao walikamatwa baada ya polisi kupata taarifa za kiinterejinsia kuhusu kujihusisha na dawa hizo za kulevya.

Ilidaiwa kuwa polisi kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa huo, walifanya upekuzi katika makazi ya washitakiwa hao ambapo walikuta bangi hiyo ikiwa imewekwa katika viloba vitano na madumu mawili.

Chanzo: Mwananchi