Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka minne jela kwa kuiba fedha za mafuta

Hukumu Pc Data Jela miaka minne jela kwa kuiba fedha za mafuta

Tue, 26 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu Najibu Bajwahuzi(33) na Shadia Joseph(32) kutumikia kifungo cha miaka minne jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa Sh852 milioni.

Banjwahuzi na Shadia ni wasimamizi wa kituo mafuta cha Sasa Kazi, kilichopo Mtoni Mtongani, Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.

Mbali adhabu hiyo, Mahakama hiyo imewaamuru kulipa fidia ya Sh400 milioni kila moja fedha ambazo wanadaiwa kuiba wakati wakiwa watumishi wa kituo hicho.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumatatu, Julai 25, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, baada Mahakama kuwatia hatia katika shtaka la wizi.

Akisoma hukumu, hakimu Shaidi amesema washtakiwa kwa pamoja walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kula njama na wizi wa fedha taslimu Sh852.02 milioni.

Hakimu Shaidi amesema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi nane wa upande wa mashtaka, Mahakama ineweza kuthibitisha shtaka la wizi, huku shtaka la kula njama, upande wa mashtaka wakishindwa kuthitisha.

 "Sasa kutokana na mahakama kuwatia hatiani katika kosa la wizi, Mahakama hii inawahukumu kifungo cha miaka minne kila mmoja na pia mnatakiwa kulipa fidia ya Sh 400milioni kila mmoja ili ifidie kiasa cha Sh852 milioni mlichoiba," amesema hakimu Shaidi.

Awali, wakili wa Serikali Mwandamizi, Christine Joas akishirikiana na Adolf Verandumi, waliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya washtakiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaoaminiwa na waajiri wao na wao kushindwa kuwa waaminifu.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mahakama iliwapa nafasi washtakiwa hao kwanini isiwape adhabu, hata hivyo washtakiwa hao waliomba wapunguziwe adhabu kwa sababu wanategemewa na familia zao.

Hata hivyo, Hakimu Shaidi ametupilia mbali maombi hayo ya washtakiwa kwa kuwahukumu kutumikia adhabu hiyo.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja walikuwa wanakabiliwa na kesi ya Jinai namba 67/2021 yenye mashtaka mawili.

Katika shtaka la kwanza,  kati ya January 2018 na Machi 26, 2020 katika kituo Cha kuuzia mafuta( Sheli) cha Sasa Kazi, kilichopo Mtoni Mtongani, washtakiwa kwa pamoja walikula njama za kutenda kosa.

Shtaka la pili, siku na eneo hilo, washtakiwa kwa pamoja wakiwa wafanyakazi wa kituo hicho cha mafuta, waliiba fedha taslimu Sh 852, 024, 698 mali ya kituo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live