Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 60 kwa kumpa mimba mwanafunzi

Jela Miaka 60 Kwa Kumpa Mimba Mwanafunzi Jela miaka 60 kwa kumpa mimba mwanafunzi

Fri, 14 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana Shinen Abdul (30) mkazi wa Kijiji cha Singa, Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela kwa kosa la kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu.

Tukio hilo lilitokea Disemba 15, 2023 katika Kijiji cha Singa, kata ya Kinampundu, Tarafa ya Nduguti, Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida ambapo mshtakiwa alimbaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka 17 .

Kufuatia tukio hilo, mshtakiwa alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa mahakamani Machi 14, 2024 ambapo Mahakama iliskiliza pande zote mbili za mlalamikaji na Mshitakiwa na kutokana ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji kujitosheleza na mshtakiwa kuridhika, Mahakama imemuhukumu Mshitakiwa kutumikia adhabu hiyo.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iramba Mhe. Luzango Omero Khamsini amesema, Mahakama imetoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa mshtakiwa na jamii kwa ujumla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live