Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 60 kwa kumpa mimba mwanafunzi

Kortini Kwa Disel Jela miaka 60 kwa kumpa mimba mwanafunzi

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, imemhukumu kifungo cha miaka 60 Jela, Faraji Milanzi Yasini (20), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Ruanda – Mkowela, wilayani Tunduru, baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi.

Akisoma hukumu hiyo kesi namba 62 ya mwaka 2023, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Honorius Kando alisema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 10, 2022 Kijiji cha Ruanda -Mkowela ambapo amehukumiwa miaka 30 kwa kila kosa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live