Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 5 kwa kujifanya Mkurugenzi Mkuu Usalama wa Taifa

USALAMA FEKI Jela miaka 5 kwa kujifanya Mkurugenzi Mkuu Usalama wa Taifa

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi imemhukumu Raymond Bwire (28) kifungo cha miaka mitano jela kwa kujifanya mkurugenzi mkuu idara ya usalama wa taifa.

Hakimu mkazi wa wilaya Mlele, Bilal Ahmed ametoa hukumu hiyo juzi baada ya kesi namba 90 ya mwaka 2022 kusikilizwa mahakamani ambapo mshtakiwa amekutwa na hatia ya kutenda kosa hilo hivyo kuhukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, mwendesha mashtaka alisema kuwa Bwire ni mkazi wa kamguluki mkoa wa Mara alikamatwa na polisi kwa kosa la kutuma ujumbe mfupi kwenye simu ya mkononi kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mlele Theresia Irafy akimtaka kumsaidia mdogo wake kupata kazi ya utendaji wa kijiji huku akijitambulisha kuwa ni mkurugenzi mkuu idara ya usalama wa taifa.

Mwendesha mashtaka huyo pia aliongezea kwa kusema kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa Agosti 12 mwaka huu akiwa mkoani Mara iliyopo katika kanda ya ziwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live