Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 5, faini milioni 20 kwa kutumia maudhui ya DStv

Dstv Kortii.jpeg Jela miaka 5, faini milioni 20 kwa kutumia maudhui ya DStv

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Karagwe imewahukumu watu wawili ambao ni David Peter Sembosi na Sebastian John kifungo cha miaka 5 jela au kulipa faini ya shilingi milioni 20 kwa kosa la kusambaza maudhui ambayo ni mali ya DStv bila kibali na ikiwa pia ni kitendo kinachokwenda kinyume cha sheria ya Hakimiliki na makosa ya kimtandao.

Uchunguzi uliofanywa na kitengo cha makosa ya mtandao ulibaini kuwa tovuti (website) hiyo inayoendeshwa kitaalamu haikutazamwa nchini Tanzania pekee bali katika hata kwenda Nchi nyingine na hutembelewa na Wateja 200,000 kila mwezi wanaopata huduma za DStv isivyo halali.

Ukiukaji wa hakimiliki nchini Tanzania unarudisha nyumba biashara ya utangazaji kwa kiasi kikubwa kwani Wawekezaji wanashindwa kupata faida inayotarajiwa kwenye uwekezaji pamoja na hasara kubwa ya mapato ya Serikali kwa kuwa uharamia wa maudhui ni kinyume cha sheria na Maharamia hao hawana leseni hivyo hawalipi ushuru wowote wa Serikali.

Akizungumzia matokeo ya kesi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MultiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso amesema;

"Tumefurahishwa na uamuzi huo na tunaamini kwamba Vyombo vyetu vya sheria vitaendelea kuhakikisha kuwa sheria zinatekelezwa kwa faida sio tu ya Waendeshaji lakini pia Serikali na tasnia ya ubunifu ya Afrika kwa ujumla na kwamba hukumu hii ni onyo kwa wote wanaohusika na vitendo vya uharamia wa maudhui kwani msako bado unaendelea," amesema Woiso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live