Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 40 kusafirisha dawa za kulevya

Jela (1) Jela miaka 40 kusafirisha dawa za kulevya

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: ippmedia.com

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara imewahukumu watu wawili kati ya watatu kifungo cha miaka 40 jela na kulipa faini ya Sh. 1,517,853,318 baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.

Hukumu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam aliyeteuliwa kusikiliza kesi hiyo, Jaji Issaya Halfani, baada ya kuridhishwa pasio shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.

Waliohukumiwa ni Ahmadi Nyamvi na Athumani Mohamedi wakazi wa Wilaya ya Kindondoni mkoani Dar es Salaam, huku ikimwachia huru mshtakiwa wa tatu, Monicar Mathias Murumba, baada ya kutoonekana na hatia.

Baada ya kutiwa hatiani, wakili aliyekuwa anawatetea, Hadson Ndusiao, aliiomba mahakama kuwapa wateja wake adhabu nafuu kwa alichodai ni wakosaji wa mara ya kwanza, pia wamekaa mahabusu kwa muda mrefu, hivyo wanajutia makosa waliyoyafanya na watakuwa raia wema warudipo uraiani.

Jaji Halfani akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 04/2012, alisema kosa la kwanza la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin aliwahukumu kila mmoja kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kulipa faini ya Sh. 1,490,780,580.

Kosa la pili la kusafirisha dawa ya kulevya aina ya cocane aliwahukumu kutumikia kifungo kama hicho jela na kulipa faini ya Sh. 13,535,869 kila mmoja na kufanya ya faini ya Sh. 1,517,853,318.

Jaji Halfani alisema adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, hivyo watalazimika kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja, huku ikimwachia huru mshtakiwa wa tatu Monica Mathias Mulumba.

Awali ilidaiwa na Mwanasheria wa Serikali, Godfey Mramba, kuwa washtakiwa walikamatwa Januari 11, 2012 katika Kijiji cha Mchinga, Wilaya na Mkoa wa Lindi, wakiwa wanasafirisha dawa hizo zikiwa kwenye madumu na thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 9.

Chanzo: ippmedia.com