Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa wizi wa mifugo

FB IMG 1671560748418 Jela miaka 30 kwa wizi wa mifugo

Tue, 20 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 Jela mkazi mmoja wa wilayani Kaliua akifahamika kwa jina la Samuel John maarufu Jaruo baada ya kutiwa hatiani kwa kosa na kuiba ng’ombe wapatao 25 akitumia silaha za jadi kuitishia familia ya mmiliki wa mifugo hiyo Nzuga Charles mkazi wa Kijiji cha Malanga wilayani Kaliua.

Aidha katika shauri hilo namba 58 la mwaka 2021 lililowajumuisha watu wengine wawili ambao mmoja Said Nasibu ambaye amefungwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kununua ng’ombe hao huku Mahakama ikimwachia huru William Jacob ambaye alitumwa kuswaga ng’ombe hao baada ya kuibwa na Samuel John kupelekwa kwa mnunuzi Said Nasibu.

Akisoma hukumu hiyo ya kutumikia kifungo cha miaka 30 Jela Hakimu mkazi Jovit Kato alisema mahakama baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili imejiridhisha pasi na shaka yoyote kwamba mshtakiwa Said John maarufu Jaruo kati ya washtakiwa watatu waliosomeka katika shauri hilo la jinai namba 58 la mwaka 2021 amehusika moja kwa moja kutenda kosa hilo huko katika Kijiji cha Malanga wilayani Kaliua.

Akisoma maelezo ya awali katika Shitaka hilo Wakili wa Serikali Alice Thomas aliiambia mahakama mshitakiwa Samuel John baada ya kutenda kosa hilo la kuvamia nyumbani kwa Nzuga Charles na kuiba Ng’ombe hao 25 wenye thamani ya Shilingi million 18 na kisha kutoweka na alipotafutwa na askari Polisi alipatikana akiwa amekamatwa tena huko Kibondo mkoani Kigoma kwa kosa jingine la kuiba ng’ombe jambo ambalo aliielezea mahakama kwamba mtu huyo ni mzoefu kulingana na makosa yanayomkabili.

Washitakiwa wenza katika shauri hilo la Jinai Said Nasib aliyenunua ng’ombe hao amehukumiwa kutumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja huku Mahakama ikimwachia huru William Jacob ambaye alitumwa kuwaswaga ng’ombe hao akiahidiwa kupata ujira kutoka kwa Samuel John.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live