Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa unyang'anyi wa iPhone

HUKUMU Jela miaka 30 kwa unyang'anyi wa iPhone

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam, imewahukumu Victor Gidio (24) na mwenzake Salehe Kilima (25) kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Gidio, mkazi wa Kijichi wilayani Temeke na Kilima anayeishi Tabata Aroma wilayani Ilala walikuwa wanakabiliwa na shtaka moja la ung'anyanyi wa kutumia silaha na kujipatia simu aina ya iphone 11 yenye thamani ya Sh1.2 milioni mali ya Edna Hebron.

Hukumu hiyo imetolewa, jana Ijumaa Desemba 22, 2023 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Aaron Lyamuya wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kusomewa hukumu.

Akisoma hukumu hiyo, iliyoandaliwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Rhoda Ngimilanga aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, Hakimu Lyamuya amesema washtakiwa wametiwa hatiani kama walivyoshtakiwa.

“Nimepitia maelezo ya mashahidi watano waliotoa upande wa mashtaka na wamethibitisha pasi na shaka kuwa washtakiwa wana hatia katika kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha, hivyo wanatakiwa kupewa adhabu,” amesema Hakimu Lyamuya.

Baada ya kueleza hayo, Lyamuya amewapa nafasi washtakiwa kujitetea kwa nini wasipewe adhabu kali na Mahakama hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao walijibu kuwa hawana cha kusema.

“Kwa mujibu wa sheria, adhabu iliyopo kwa kosa hili ni moja tu, nayo ni kifungo cha miaka 30 jela, Mahakama inawahukumu kila mmoja kifungo cha miaka 30 jela,” amesema Lyamuya.

Muda mfupi baada ya Mahakama hiyo kuwahukumu kifungo hicho, washtakiwa hao waliokuwa wamesimama waliinama chini na kuanza kutoa machozi.

Awali, wakili wa Serikali Pancrasia Protas, aliomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 10, 2022 eneo la uwanja wa ndege, lililopo jijini Ilala.

Siku hiyo, Gidio na Kilima, waliiba simu aina ya iphone 11 ya Sh 1.2milioni, mali ya Edna Hebron.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live