Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa kusafirisha heroin

2aac5a800b955791fce136728f8038ce Jela miaka 30 kwa kusafirisha heroin

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu miaka 30 jela Linna Maro (47) kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 43.95.

Pia Mahakama hiyo imetaifisha simu nne za mfanyabiashara huyo alizokutwa nazo.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Agustina Mbando wa mahakama hiyo baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kuthibitisha pasipo shaka yoyote kuwa mshtakiwa alikamatwa na dawa za kulevya anazotuhumiwa nazo.

Linna alikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Januari 26, 2018 eneo la Tabata Bima Jijini Dar es Salaam, akiwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya aina ya heroin na kufunguliwa kesi ya jinai.

Alisrema mshtakiwa huyo ametiwa hatiani kwa kufanya biashara ya dawa za kulevya kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 5 ya mwaka 2015.

Chanzo: habarileo.co.tz