Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi

Jela 1?fit=660%2C330&ssl=1 Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkulima Stanford Theobert (19) mkazi wa Maporomoko, Tunduma, kwa kosa la kumbaka mwanafunzi baada ya kumdanganya mwanafunzi huyo kuwa atamuoa.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa Januari 23, 2023 maeneo ya Kata ya Maporomoko Mjini Tunduma ambapo alituhumiwa kumdanganya kuwa atamuoa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 na kumbaka jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha 130 (2) (e) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16 ya mwaka 2022.

Akisoma maelezo ya hukumu ya kesi hiyo yenye kesi namba 23/2023 Hakimu mkazi wa Wilaya ya Momba Timothy Lyon alisema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa la kubaka na kumhukumu adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine

Chanzo: www.tanzaniaweb.live