Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi

Kortini Geita.jpeg Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mangode Rajabu (23),Mkazi wa Soga,Kibaha kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi (jina linahifadhiwa).

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 4/ 2023 imetolewa Jana na Hakimu Fahamu Kibona wa mahakama ya Wilaya ya Kibaha wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Fahamu Kibona alieleza amejiridhisha kumtia hatiani mshitakiwa huyo kwa Mujibu wa kifungu 130 (1), (2) (a) na kifungu 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Ilielezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Novemba 7,2021 huko Soga,Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live