Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi

29355 Serengeti+picTanzaniaWeb

Thu, 29 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mkazi wa kijiji cha Nyichoka wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Peter Wangwe (18) huenda akatimiza umri wa utu uzima akiwa gerezani akitumikia kifungo cha miaka 30 alichohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Serengeti kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 13.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumatano Novemba 28, 2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile baada ya kuridhika na ushahidi wa Jamhuri uliotolewa na mashahidi watano kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Kabla ya kupewa adhabu hiyo ambayo hakimu Ngaile amesema ndio ya chini kulinganisha na ile ya kifungo cha maisha, mshitakiwa aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu akisema hilo ndilo kosa lake la kwanza, utetezi ambao haukumuepusha na adhabu.

Awali, mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Paskael Nkenyenge aliieleza mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 3, 2017 akiwa katika kijiji cha Nyichoka wilayani Serengeti.

Katika tukio hilo, mshtakiwa anadaiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka 13 ambaye wakati huo alikuwa akisoma shule ya msingi.

“Kosa hilo ni kinyume na kifungu 130 (1) (2) (e) na kifungu 131 (1) kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,” amesema Nkenyenge.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz