Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto

Thu, 6 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Makahama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkazi wa Chemchem manispaa ya Tabora, Patrick Kabula (24) kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka mitano.

Adhabu hiyo imetolewa leo na Hakimu Joctan Rushwela baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa Jamhuri.

Hakimu Rushwela amesema anatoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia za kikatili kwa watoto.

Awali,  upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali,  Idd Mgeni ulidai Februari 12 mwaka huu eneo la Mwinyi, mshtakiwa akiwa nyumbani kwake alimbaka mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali.

Alidai mshitakiwa alimtisha mtoto huyo asiseme kwa mtu yeyote na akithubutu angemuua.

Alisema mama wa mtoto huyo alibaini mwanaye kufanyiwa kitendo hicho cha kikatili wakati akimuogesha.

Wakili huyo aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na wengine.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz