Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa kumbaka mfanyakazi wake wa ndani

Pingu Selo 660x400 Jela miaka 30 kwa kumbaka mfanyakazi wake wa ndani

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Mwananchi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mkazi wa Miembesaba mkoani humo, Otienal Ibrahimu (36), baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mfanyakazi wake wa ndani mwenye umri wa miaka (15).

Hukumu hiyo imetolewa Julai 31, 2023 na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Fahamu Kibona huku upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Elizabeth Olomi, akisaidiana na Asifiwe Mzava na upende wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Iddi Msawanga.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, ilielezwa kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 15, 2023 alfajiri nyumbani kwao huko Miembesaba, baada ya mke wake kuelekea kazini na hivyo mdaiwa kutumia mwanya huo kutekeleza unyama huo.

Ilielezwa kuwa siku hiyo mshtakiwa huyo alimfuata mfanyakazi wake chumbani huku akiwa amevaa taulo na pesa mkononi kiasi cha Sh20,000 akitaka kumpatia ili amkubalie kufanya naye mapenzi, jambo ambalo msichana huyo hakuliafiki na hivyo Danielic kumshika kwa nguvu na kumbaka.

“Baada ya kutekeleza kitendo hicho, mfanyakazi wake alimueleza mke wa mshtakiwa aliporejea kutoka kazini, lakini pia aliwasiliana na baba yake aishie mikoani na hata kuwaeleza rafiki zake waishio kwenye eneo hilo ambao walilivalia njuga suala hilo na kuripoti kituo cha polisi,” amesema Hakimu kibona.

Amesema kuwa baada ya taarifa kufika polisi msako ulianza na kwamba mshitakiwa alikimbilia mkoani Dodoma, hata hivyo alikamatwa na Polisi Juni 9, 2023 na hivyo kufikishishwa mahakamani kuendelea na kesi hiyo.

Imeelezwa kuwa mahakama hiyo ilifikia hatua ya kumhukumu adhabu hiyo baada ya kuridhishwa pasipo na shaka na ushahidi uliotolewa na daktari na mwathirika wa tukio hilo, huku mshitakiwa akijitetea kuwa siku ya tukio hilo hakuwepo nyumbani ingawa utetezi wake huo haukumnusuru na adhabu hiyo ya miaka 30 jela.

Chanzo: Mwananchi