Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa kubaka Mwanae wa kufikia

Jela Pc 660x400.jpeg Jela miaka 30 kwa kubaka Mwanae wa kufikia

Sat, 22 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkazi wa Kijiji cha Buchanchari wilayani Serengeti, Chegera Mayemba amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka mtoto wake wa kufikia.

Mayemba (35) amepewa hukumu hiyo na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti, Judith Semkiwa baada ya kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.

Mbali na ushahidi huo, pia mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo ambapo, Hakimu Semkiwa amesema kosa hilo adhabu yake ni miaka 30 jela huku akiacha wazi milango ya rufani.

Awali, Wakili wa Serikali na ambaye ni Mkuu wa Mashitaka Wilaya ya Serengeti, Mafuru Moses ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 12, mwaka huu.

Amesema baada ya kupitia jalada na kubaini ushahidi wa tukio hilo uko wazi kuwa Mei 21, mwaka huu, wamemfikisha mahakamani na baada ya kusomewa na kukiri akaomba mahakama kutoa adhabu kali kwa kuwa kitendo alichofanya ni cha kinyama.

MTOTO JASIRI ANATANGAZA DW, AWASHANGAZA WENGI, ANA UWEZO WA AJABU, AJIZOLEA UMAARUFU MKUBWA DUNIANI

Chanzo: millardayo.com