Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa kubaka

Hukumu Pc Data Jela miaka 30 kwa kubaka

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Masanja Bulagobe (49) mkazi wa Kijiji cha Zagayu wilayani humo kwa kosa moja la kubaka.

Katika kesi hiyo namba 3474 ya mwaka 2024 chini ya Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama hiyo, Robert Kaanwa, mbali na adhabu hiyo mtuhumiwa alitakiwa pia kumlipa fidia mhanga kiasi cha Sh 300,000.

Awali akielezea mahakama kabla ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya taifa ya mashtaka ya wilaya, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Jaston Mhule alieleza kuwa mnamo Januari 30, 2024 mshtakiwa alimbaka mwanamke mmoja (32) mkazi wa kijiji jirani cha Sasago.

Mwendesha Mashtaka huyo amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130 (1), (2) na 131(1) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ambavyo ilifanyiwa marejeo mwaka 2022.

Ameendelea kwa kueleza kuwa mshtakiwa siku ya tukio, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo majira ya usiku na kukuta akiwa amelala na watoto wake huku mme wa mwanamke huyo ikielezwa alikuwa amesafiri siku hiyo.

Amesema mtuhumiwa baada ya kufika nyumbani kwa mwanamke huyo, alisukuma mlango na kuingia ndani, kisha akamshikia panga mwanamke huyo ili asipige kelele na baadaye kumbaka.

Jumla ya mashahidi watano walitoa ushahidi wao katika kesi hiyo na kielelezo kimoja kutolewa kama ushahidi, ambapo mahakama ilimkuta na hatia huku akiomba Mahakama kumpungizia adhabu kwa sababu ana familia inamtegemea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live