Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 30 kwa kosa la ubakaji

Jela 1?fit=660%2C330&ssl=1 Jela miaka 30 kwa kosa la ubakaji

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mkazi mmoja wa kijiji cha Imalinyi kilichopo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe Anania Mbangule (24) amehukumiwa miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka binti wa umri wa miaka 17.

Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya wilaya ya Njombe, Matrida Kayombo amesema mshtakiwa huyo pia amehukumiwa miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya kumtorosha binti huyo.

Amesema matukio yote mawili yalitokea tarehe 24 mwezi Juni mwaka huu katika mtaa wa Kitisi uliopo Makambako wilayani Njombe.

Amesema siku hiyo ya tukio mshtakiwa alimteka binti huyo na kufanya nae mapenzi bila ya ridhaa yake ambapo ni kinyume cha sheria kifungu 130(1)(2)(e) na 131(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2019.

"Kosa hili la kumtorosha mhanga pia lina kifungo ambacho atahukumiwa nacho cha miaka saba jela" amesema Kayombo.

Wakili wa serikali aliyeendesha shauri hilo la jinai namba 66/2021 Rehema Mpagama alisema kwa kuwa mshtakiwa huyo kosa hilo amelifanya kwa mara ya kwanza ila apewa adhabu kwa mujibu wa sheria.

Advertisement "Pamoja na kuwa kosa hili ni la kwanza kwa mshtakiwa tunaiomba mahakama kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria" amesema Rehema.

Katika utetezi mshtakiwa aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana watu ambao wanamtegemea kwasasa.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz