Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 20 kwa kukutwa na ngozi ya Chui

Chui Mk Jela miaka 20 kwa kukutwa na ngozi ya Chui

Wed, 15 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara imemuhukumu John Simon (42) mkazi wa Dareda Babati kifungo cha miaka 20 kwenda jela kwa kosa la kukutwa na ngozi ya Chui ambayo thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni 8.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo 19/02/2021 katika Kijiji cha Mandi Babati ambapo wakili wa serikali Grace Mgaya amesema mshtakiwa huyo John Simon alimtegeshea Felisian Mobeshi (57)ngozi hiyo ya Chui kwenye mahindi na kisha kuipeleka nyumbani kwa Felisian na baadae kutoa taarifa Polisi.

Mgaya amesema baada ya uchunguzi imeonekana kuwa mshtakiwa John Simon sio mara yake ya kwanza kutegeshea wenzake nyara za Serikali na baadaye kutoa taarifa Polisi kwamba Wahusika wamekutwa na nyara hizo za Serikali kwa lengo la kijipatia kiasi cha shilingi laki moja.

Pia Wakili Mgaya amesema Mshtakiwa huyo amekuwa akitumwa na Mtu aliyefahamika kwa jina la Petro Damas kuweka mitego hiyo kwa Watu ambao amegombana nao kwa lengo la kuwakomesha na baadae kulipwa laki moja baada ya kutekeleza agizo hilo.

“Amekuwa anatumwa kwenda kutegesha mitego(nyara za Serikali) kwa Watu ambao wamekuwa na kutokuelewana na Petro Damas alafu yeye mwenyewe anapiga simu Polisi kutoa taarifa akieleza kwamba nyumba fulani kuna nyara za serikali sehemu fulani ambapo kiuhalisia nyara hizo anakuwa ametegesha yeye mwenyewe kwa tamaa ya kupata laki moja aliyoahidiwa lakini mwenzake huyo Petro Damas amekimbia kusiko julikana,” Mgaya.

Hukumu hiyo imetolewa jana June 13 katika Mahakama hiyo ya wilaya na hakimu Victor Kimario kwenda jela miaka 20 ila mshtakiwa anayo haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live