Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 20 kwa kukamatwa na meno ya tembo

Meno Ya Tembo Meno ya tembo

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara imemuhukumu Gurtu Sirro (33) Mkazi wa Sarame Magugu kifungo cha miaka 20 kwenda jela baada ya kukutwa na meno matatu ya Tembo ambayo thamani yake ni zaidi ya shilingi Milioni 45.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu wa Mahakama hiyo Victor Kimario ambapo amesema Sirro alikamatwa January 17,2023 katika Kijiji cha Mafuta akiwa na meno matatu ya Tembo ambayo ni nyara za Serikali.

Waendesha mashtaka wa Serikali katika kesi hiyo Rusticus Mahundi na Abood Komanya wamesema Mshtakiwa hana rekodi zozote za matukio kama hayo hivyo wameiomba Mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa Watu wengine wenye tabia kama hizo huku Mshtakiwa (Gurtu Sirro) akiiomba Mahakama imuondolee adhabu hiyo kwa kuwa anategemewa na Watoto wanne ambao Mama yao hawezi kufanya kazi hivyo wanamtegemea yeye pekee.

Hakimu Kimario amesema Mshtakiwa anayo haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30 kuanzia leo huku akiagiza meno hayo ya Tembo ambayo yalitumika kama kielelezo namba moja kukabidhiwa kwa Afisa Wanyamapori wa Wilaya ili kuyapeleka sehemu husika kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live