Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 15 kwa kuua bila kukusudia

HUKUMU Jela miaka 15 kwa kuua bila kukusudia

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Ismail Ndage (27) kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Beatrice Onesmo kwa kumchoma kisu tumboni.

Hukumu hiyo imetolewa Desemba 7, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo, baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani mshtakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia.

"Nimepitia ushahidi wa upande wa mashtaka akiwemo daktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke, ambaye aliumfanyia uchunguzi mwili wa Beatrice na kubaini kuwa chanzo cha kifo chake ni mapafu kujaa hewa iliyoingia kupitia njia isiyo rasmi na kusababisha mapafu kuwa meusi na kupelekea kuvuja damu nyingi.

“Hivyo Mahakama hii inakuhukumu kifungo cha miaka 15, jela ili iwe fundisho kwako na vijana wengine," amesema Hakimu Mazengo.

Ndage anadaiwa kumuua Onesmo, baada ya kupigiwa kelele za mwizi katika nyumba ya Editha Alphonce, eneo la Tandika Azimio, alipolazimisha apewe simu na hela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live