Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 10 kwa kutafuna muamala aliotumiwa kimakosa

Tumbua Tena Mwamba Jela miaka 10 kwa kutafuna muamala aliotumiwa kimakosa

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Steven Fields wa Georgia nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela miaka 10 kwa kosa la kutumia sehemu ya pesa zilizotumwa kimakosa kwenye account yake ya benki.

Maofisa wa Usalama wamesema Steven alishtakiwa kwa kosa la wizi baada ya muhudumu wa Benki kumuwekea kimakosa hundi ya $31,000 kwenye akaunti yake, hundi ambayo ilitakiwa kwenda kwa mteja mwingine ambaye wanafanana majina (Steven Fields).

Taarifa zinadai kuwa baada ya kupokea hiyo pesa kijana huyo alitoa $20,000 (Tsh 46,640,000) kwenye akaunti hiyo na kufanya miamala mingine ya $5,000 (Tsh 11,660,000) kwa kutumia kadi yake ya benki

hakuishia hapo tu, kesho yake Steve alirudi tena kutaka kuchukua pesa nyingine lakini Benki ikawa imeshtuka na kuwaita Polisi.

Imeelezwa kwamba, Steven alitumia pesa hizo ‘kujitunuku’ gari aina ya BMW convertible.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live