Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela miaka 10 kwa kucheza hadharani

IRAN KUCHEZA HADHRANI (600 X 355) Jela miaka 10 kwa kucheza hadharani

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Iran imewahukumu kifungo cha kila mmoja miaka 10 na miezi sita Jela Wapenzi wawili ambao walionekana kucheza mbele ya moja ya alama kuu za Jiji la Tehran, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za Iran.

Astiyazh Haghighi na Mchumba wake, Amir Mohammad Ahmadi, wote wakiwa na umri wa miaka 20, walikamatwa mwezi November mwaka jana baada ya video kusambaa ikiwaonesha wakicheza kimahaba mbele ya Mnara wa Azadi.

Haghighi hakuwa amevaa hijabu, kikiwa ni kitendo ambacho ni kinyume na sheria kali za Iran, Wanawake pia hawaruhusiwi kucheza hadharani hata wakiwa wenyewe achilia mbali kucheza na Wanaume.

Mahakama ya mjini Tehran imewahuhukumu kila mmoja kifungo cha miaka 10 na miezi sita jela, pamoja na kuwekewa marufuku ya kutumia mtandao na kuondoka Iran, Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu (HRANA) lenye makao yake makuu nchini Marekani limesema.

Wapenzi hao, ambao tayari walikuwa na Wafuasi kadhaa Jijini Tehran kama Watu maarufu wa Instagram, walitiwa hatiani kwa kuhimiza ufisadi na ukahaba wa umma na kuwa na nia ya kuvuruga usalama wa Taifa hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live