Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela maisha kwa kumbaka mwanae wa mwaka mmoja

Jela Miaka 52 Kwa Kumuua Mtoto Miaka 5 Kwa Tambiko Jela maisha kwa kumbaka mwanae wa mwaka mmoja

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama wilayani Mbogwe mkoani Geita imemhukumu kifungo cha maisha jela Mabula Maduhu mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Kijiji cha Shinyanga A wilayani Mbogwe mkoani Geita kwa kosa la kumbaka mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita ACP Safia Jongo, amesema tukio hilo la ubakaji linahusishwa na imani za kishirikina.

"Mganga alimshauri ambake mtoto wake mdogo ambapo alikuwa na mtoto wake mwenye mwaka mmoja na nusu alivyorudi nyumbani akamtuma mkewe sokoni akamwambia mwache mtoto niwe ninamwangalia.

"Mama alivyorudi ndo akakutwa mtoto yule amebakwa tulipomkamata alikiri kufanya ukatili huo kwamba ameshawishiwa na mganga wa kienyeji kwamba akifanya hivyo ndio njia ya mafanikio yake," amesema ACP Jongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live