Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuhukumu, Stambuli Yusufu (35) kifungo cha maisha jela baada ya kumkuta na hatia ya kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wa kike wa miaka nane.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo anayesoma darasa la nne kati ya mwaka 2017 na 2018.
Imeelezwa kuwa baada ya kitendo hicho alikuwa akimpatia Sh1,000 hadi 2,000, kumtaka asiseme kwa mtu yeyote.
Akisoma hukumu hiyo leo Jumanne Januari 28, 2020 hakimu mkazi, Jimson Mwankenja amesema kifungo cha maisha jela kitaanza kuhesabiwa baada ya mshtakiwa kumlipa Sh2 milioni mtoto huyo.
Amesema ikiwa atashindwa kulipa fidia hiyo, atachapwa viboko 12 na kuanza kutumikia kifungo hicho.
Hakimu Mwankenja amesema ametoa hukumu hiyo baada ya kuzingatia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka, utetezi wa mshtakiwa na uzito wa kosa hilo.
Pia Soma
- Mama wa bilionea Msuya aomba suluhu nje ya mahakama
- Kesi ya Zitto uteuzi wa CAG yaanza kutajwa
- Wanaodahili wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya Tanzania wapewa miezi mitatu
Amesema katika kesi hiyo, kwenye hati ya mashtaka waliandika kifungu cha 154(1) na (2) bila ya kuainisha kama kilifanyiwa marekebisho na kifungu cha 16 cha makosa ya kujamiiana namba 4 ya 1998.