Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela maisha kwa kumbaka binti wa miaka 13

Mbakaji Maisha Jela maisha kwa kumbaka binti wa miaka 13

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Kijiji cha Mhunze, kilichopo Halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga, Hamza Butondo amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kumbaka binti wa miaka 13.

Hakimu Mkazi Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Zahoro amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 11, 2022 majira ya saa 10 alfajiri katika Kijiji cha Mhunze ambapo ilielezwa mahakamani hapo kuwa aliingia ndani ya nyumba alipokuwa binti huyo na kumtishia kumchoma kisu kabla ya kutekeleza kitendo hicho.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Jukael Jairo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo huku akijua kuwa ni kosa, na kumsababishia madhila mhanga huyo na kuomba mahakama itoe adhabu kali, kwani mtuhumiwa amekuwa tishio kwa wakazi wa Kishapu na kwamba Mkoa wa Shinyanga umekuwa ni miongoni mwa mikoa yenye matukio mengi ya ukatili wa kijinsia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live