Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela maisha kwa kubaka mtoto wa chekechea

Jelaa2.png Jela maisha kwa kubaka mtoto wa chekechea

Fri, 26 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Iringa aitwaye Charles Kasuke (29) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa jirani yake mwenye umri wa miaka 6 aliyekuwa akisoma shule ya awali (chekechea).

Mtuhumiwa huyo mkazi wa Kilolo, Ruaha Mbuyuni aliyekuwa akijishughulisha na kazi ya kinyozi inadaiwa kuwa mnmo Februari 24, 2023 alimuita mtoto huyo na kumuingiza kwenye nyumba ambayo haijaisha ‘pagale’ na kumbaka.

Baada ya mama wa mtoto huyo kufuatilia, mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa vile alikuwa akiishi karibu na nyumba yao na wanamfahamu vizuri.

Kesi hiyo ilikuwa na mashahidi nane wakiwemo baba na mama wa mtoto, mtoto mwenyewe, askari wa upelelezi, daktari aliyempima mtoto huyo na kubaini kuwa alikuwa ameingiliwa kimwili.

Baada ya kupewa nafasi ya kujitetea, mtuhumiwa huyo alisema kuwa anakusudia kukata rufaa, ndipo mahakama ilipomhukumu kwenda jela maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live