Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela Miaka 30 kwa Kubaka Mtoto Wake

Jela Kubaka?fit=860%2C539&ssl=1 Jela Miaka 30 kwa Kubaka Mtoto Wake

Sat, 22 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

MKAZI wa Kijiji cha Buchanchari wilayani hapa, Chegera Mayemba amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka mtoto wake wa kufikia.

Mayemba (35) amepewa hukumu hiyo jana Ijumaa Mei 21, 2021 na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti, Judith Semkiwa baada ya kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.

Mbali na ushahidi huo, pia mshitakiwa alikiri kutenda kosa hilo ambapo, Hakimu Semkiwa amesema kosa hilo adhabu yake ni miaka 30 jela huku akiacha wazi milango ya rufani.

Awali, Wakili wa Serikali na ambaye ni Mkuu wa Mashitaka Wilaya ya Serengeti, Mafuru Moses ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 12, mwaka huu.

Amesema baada ya kupitia jalada na kubaini ushahidi wa tukio hilo uko wazi kuwa Mei 21, mwaka huu, wamemfikisha mahakamani na baada ya kusomewa na kukiri akaomba mahakama kutoa adhabu kali kwa kuwa kitendo alichofanya ni cha kinyama.

Chanzo: globalpublishers.co.tz