Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jela Maisha kwa kumbaka mtoto wake wa kambo

RUNGU Fadhili alimbaka mtoto wake wa kambo mwenye miaka 8

Fri, 29 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe imemuhukumu Fadhili Ngoho (25) mkazi wa Ulembwe, Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe kwenda jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Mtoto wa miaka 8.

Fadhili amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka Mtoto wa miaka 8 ambaye ni Mtoto wake wa kambo aliyekuwa akisoma katika moja ya shule ya msingi iliyopo katika kata ya Ulembwe

Inaelezwa kuwa siku hiyo Mshtakiwa alimbaka Mtoto huyo na kumwambia asipige kelele "Tarehe 23/2/2020 Mama wa Mtoto huyo alimuona Mwanae hatembei vizuri ndipo alipomuuliza ana tatizo gani na kisha Binti huyo akamwambia Mama yake kuwa Baba yake wa kambo alimbaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live