Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jasusi maarufu Marekani aachiwa huru baada ya miaka 20

Ana Montes Jasusi maarufu Marekani aachiwa huru baada ya miaka 20

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ana Montes ni miongoni mwa majasusi maarufu wa Vita Baridi waliokamatwa na Marekani, ameachiliwa huru baada ya kukaa gerezani kwa zaidi ya miaka 20.

Huyo mwenye umri wa miaka 65 alitumikia kifungo kwa miaka takriban miwili kwa kuipeleleza Cuba akiwa ameajiriwa kama mchambuzi katika Shirika la Ulinzi na intelijensia.

Baada ya kukamatwa mwaka 2001, mamlaka walisema alikuwa karibu kabisa kufichua oparesheni za kijasusi za Marekani katika kisiwa hicho.

Afisa mmoja alisema alikuwa miongoni mwa "wapelelezi waharibifu zaidi" walionaswa na Marekani.

Michelle Van Cleave, ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha kijasusi chini ya Rais George W Bush, aliliambia Congress mwaka 2012 kwamba Montes "alitoa ushirikiano wa karibu kila kitu ambacho tulijua kuhusu Cuba na jinsi tulivyoendesha Cuba".

"Kwa hiyo raia wa Cuba walikuwa wanafahamu kila kitu tunachokifahamu kuhusu wao na wangeweza kutumia kwa manufaa yao. Aidha, aliweza kushawishi makadirio kuhusu Cuba katika mazungumzo yake na wenzake na pia alipata fursa ya kutoa taarifa ambazo alizipata. kwa mamlaka zingine."

Baada ya kukamatwa kwake, Montes alishtakiwa kwa kutoa utambulisho wa wapelelezi wa Marekani na nyenzo za siri za baharini. Alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela, huku hakimu aliyemhukumu akimshutumu kwa kuliweka taifa hatarini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live