Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jambazi auawa akijaribu kuiba Equity Bank

Jambazi Auawa Akijaribu Kuiba Equity Jambazi auawa akijaribu kuiba Equity

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jambazi mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi huku mwenzake akijeruhiwa wakati walipokuwa wakijaribu kuiba katiba benki ya huko Equity huko Nairobi West nchini Kenya.

Tukio hilo limetokea jana Jumanne, Oktoba 11, 2022 katika eneo hilo la benki ambapo mwizi huyo aliwajeruhi kwa kuwachoma visu watu watatu wakiwemo askari wawili na mteja mmoja wa benki kabla ya Polisi wa benki hiyo kumfyatulia risasi jambazi huyo begani na tumboni.

Maafisa hao wa polisi walisema kuwa wezi hao alikuwa akijaribu kuiba pesa zilizokuwa zimeletwa kwenye benki hiyo na G4S huko Ghandi Avenue.

Kulingana na mashahidi, mwizi huyo mwingine alifanikiwa kutoroka baada ya kusababisha vurugu hiyo wakati mlinzi mmoja akiripotiwa kuwa na hali mbaya.

Barabara inayoelekea kwenye benki hiyo ya Equity imefungwa kwa muda ili kutuliza yaliyotendeka na kufanya uchunguzi wa wizi huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Nairobi James Mugera alisema polisi waliokuwa wakisimamia benki hiyo walijibu kwa kumfyatula risasi jambazi huyo begani na tumboni. Jambazi huyo pia alikimbizwa katika Hospitali ya Mabagathi, ambapo alikata roho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live