Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jambazi aliyehukumiwa miaka 30 jela akamatwa

Majambazi Muliro Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP, Jumanne Muliro

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kumkamata Johnson Omary Mchome (39) anayedaiwa kufanya vitendo mbalimbali vya uhalifu (ujambazi) kwa kutumia jina jingine,  huku rekodi zikionesha aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya unyanganyi.

Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro amebainisha kuwa Mtuhumiwa huyo alikamatwa  Novemba 24 mwaka huu maeneo ya Kwembe Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo wakati wa kukamatwa kwake, alitoa bastola yake na kuanza kuwashambulia askari.

Aidha Muliro amebainisha kuwa Mtuhumiwa huyo alikiri kufanya matukio mbalimbali ya uporaji jijini Dar es Salaam, akifafanua kuwa kwa sasa Mtuhumiwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kujeruhiwa, kwenye majibizano ya risasi na askari.

Jeshi la Polisi linaendelea kumuombea mtuhumiwa apone haraka ili aendelee na mahojino zaidi, huku likiwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live