Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamaa anaswa na simu 93

SIMU MTUHUMIWA Jamaa anaswa na simu 93

Tue, 19 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa wa Polisi katika Kaunti ya Nairobi wanamshikilia jamaa mmoja kwa madai ya wizi wa simu za mkono.

Brian Mutua Muema alikamatwa Ijumaa na maafisa kutoka kituo cha Kware, Embakasi baada ya kupatikana na simu 93.

Polisi waliofika kwenye makazi ya mshukiwa katika eneo la Pipeline walikuta aina mbalimbali za smartphones zinazoshukiwa kuwa ni za wizi.

Polisi walipokea taarifa za wizi huo kutoka kwa wananchi ndipo wakaamia wakaamua kuvamia chumba hicho ambacho jamaa alikuwa amekodi na kukuta simu hizo.

Mshukiwa alijikuta matatani baada ya kushindwa kutoa maelezo kamili ya kuthibitisha umiliki wa simu hizo.

Mara moja maafisa hao walishuku kuwa simu hizo zilikuwa zimebiwa na kumtia pingu mshukiwa.

Muema kwa sasa yuko rumande akisubiri kufikishwa mahakamani huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Mkuu wa Huduma za Taifa za Polisi iliwataka wananchi kujitolea kutoa taarifa kuhusu watu wanaowatilia shaka au shughuli zao, na kuongeza kuwa utoaji taarifa ni chombo chenye ufanisi zaidi katika vita dhidi ya uhalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live