Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada la kesi ya vigogo wa Six Telecom lakwama kwa DPP

5971 RINGO TZW

Fri, 6 Apr 2018 Chanzo: mtanzania.co.tz

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeutaka upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili vigogo wa Kampuni ya Six Telecoms Limited akiwamo Wakili maarufu Dk. Ringo Tenga.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa zamani wa Benki ya Rasilimali (TIB) Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Chacha.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakamani hiyo, Thomas Simba amesema hayo baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi Mutalemwa Kishenyi, kuieleza mahakamani hiyo kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Kishenyi alidai jalada la vigogo hao lipo mikononi mwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kuiomba mahakamani hiyo kupanga tarehe nyingine Kwa ajili ya kutajwa.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Alex Mushumbusi ulidai kuwa wakati ujao upande wa mashaka uje na sababu za msingi na kuieleza mahakama upelelezi ulipofikia.

Hata hivyo, Hakimu Simba amesema ifike mahali upande wa mashtaka uharakishe upelelezi ili washtakiwa hao kama kufungwa wafungwe.

Amesema sababu zinazotolewa mahakamani hapo za kudai upelelezi haujakamilika itafika wakati zitakwisha kwa sababu upande wa mashaka ndiyo unaounganisha mahakama na DPP.

“Sisi hatuwezi kumuona DPP bali tunaunganishwa na ninyi (upande Wa mashtaka), kwa hiyo mnapaswa kukamilisha upelelezi ili washtakiwa kama ni kufungwa wafungwe,” amesema Hakimu Simba.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 20, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: mtanzania.co.tz