Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jalada la kesi ya mke wa bilionea Msuya lipo kwa DPP

11998 Kesi+pic TanzaniaWeb

Mon, 23 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jalada la kesi ya mauaji inayomkabili Miriam Mrita, ambaye ni mke wa marehemu Erasto Msuya, na mfanyabiashara Revocatus Muyella, lipo mikononi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka  (DPP).

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita alieleza hayo leo Julai 23, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipotajwa mahakamani.

Wakili Mwita alieleza mahakamani hapo kuwa leo ilikuwa siku ya kutaja shauri hilo na kwamba jalada halisi lililopo mikononi mwa DPP, bado linafanyiwa kazi.

Baada ya wakili Mwita kueleza hayo, wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala aliomba kesi hiyo ipangiwe siku saba.

Hakimu Simba alisema upande wa mashtaka wafuatilie jalada hilo kwa kuwa limeshatoka ofisi ya DPP na kwenda mikononi mwa DPP.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Julai 30, 2018.

Katika kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2017, washtakiwa  wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth Msuya, ambaye ni dada wa tajiri huyo maarufu kwa jina la Bilionea Msuya.

Kwa mujibu wa mashtaka hayo, mauaji hayo yalifanyika Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Soma Zaidi:

Mke wa bilionea Msuya aomba korti impe nafasi ya kuonana na Rais

Februari 23, 2016, washtakiwa hao waliachiwa huru na Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mwambapa katika kesi ya mauaji namba 32 ya mwaka 2016.

Lakini baadaye walikamatwa tena na baadaye kusomewa mashtaka hayo ya mauaji upya.

Washtakiwa wapo rumande kwa sababu shtaka la mauaji linalowakabili ni miongoni kwa mashtaka yasiyo na dhamana.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz